• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima

"WAZAZI TIMIZENI WAJIBU WENU NDANI YA FAMILIA"...DC MANGOSONGO

Tarehe ya kuwekwa: May 15th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo ametoa wito kwa wazazi na walezi kutimiza majukumu yao ya msingi ndani ya familia ili kuimarisha hali ya upendo na kuepusha migogoro ya kila mara inayopelekea familia nyingi kusambaratika.

Akizungumza mbele ya wananchi waliojitokeza kwa wingi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia Duniani Jumatatu Mei 15, 2023 yaliyofanyika viwanja vya Soko Kuu Mbinga Mjini, Mkuu huyo wa Wilaya amesema familia ni taasisi muhimu katika kujenga na kuimarisha jamii na taifa kwa ujumla lakini miaka ya hivi karibuni kumekuwepo wimbi la mmomonyoko wa maadili linalotokana na wazazi na walezi kutowajibika kikamilifu katika kutimiza majukumu yao ndani ya familia.

Aidha DC Mangosongo amekemea vitendo vya ukatili vinavyotokea kwenye familia huku akikumbushia umuhimu wa kuwa na maadili mema na kujenga dhana ya upendo miongoni mwa wanafamilia na jamii kwa ujumla.

"Nawaombeni tuendelee kuisaidia na kushirikiana na Serikali katika kuibua na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia ndani ya familia na jamii zetu kwa kuhakikisha tunatoa taarifa za uwepo wa dalili na viashiria vyake kwenye mamlaka na vyombo vinavyohusika". Amesema DC Mangosongo.

Siku ya Kimataifa ya Familia Duniani huadhimishwa tarehe 15 ya kila mwaka huku mwaka huu 2023 yamefanyika katika maeneo mbalimbali nchini yakiwa na Kauli Mbiu isemayo Imarisha Maadili na Upendo kwa Familia Imara.

Akizungumzia maudhui ya maadhimisho haya Bi. Cecilia Mbata ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii amesema ni katika kutambua umuhimu wa familia kama taasisi na chanzo cha jamii yoyote duniani na kwamba kauli mbiu ya mwaka huu inakumbusha umuhimu wa kuzingatia maadili mema katika malezi na makuzi ya watoto lakini pia inasisitiza suala la upendo miongoni mwa familia na jamii.

Imeandikwa na Salum Said,

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga 

Tarehe 15 Mei, 2023

Matangazo

  • TANGAZO LA USAILI NAFASI YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU June 23, 2023
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI ENEO LA KIAMILI October 13, 2021
  • MAELEKEZO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA SHULE ZA BWENI 2023 December 18, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA MAFUNZO YA UANAGENZI KWA VIJANA March 06, 2023
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MBINGA DC NA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UGONJWA WA USUBI

    September 15, 2023
  • "WANAWAKE WA MBINGA JIKITENI KATIKA SHUGHULI ZA KIUCHUMI"MANGOSONGO

    September 14, 2023
  • WILAYA YA MBINGA YAUNDA MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI 48

    September 13, 2023
  • ELIMU YA LTIP YATOLEWA KWA WAJUMBE WA BARAZA NA KAMATI YA USIMAMIZI

    September 08, 2023
  • Tazama zote/kote

Video

MANGOSONGO ATETA NA WANANCHI FURSA ZA KIUCHUMI NANE NANE
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit