• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima

"UKIMWI BADO NI TISHIO" DC MBINGA AONYA

Tarehe ya kuwekwa: December 1st, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo amewataka wananchi wilayani humo kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara na kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika kupambana na maambukizi ya virusi hivyo hatari duniani.

Akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo kwa Wilaya ya Mbinga yamefanyika Kata ya Mpepai Mhe. Mangosongo amesema jamii ikihamasika kwa wingi katika suala la upimaji wa Virusi vya UKIMWI (VVU) na kila mmoja akachukua hatua mara baada ya kutambua hali ya afya yake itasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti kasi ya maambukizi ya virusi hivyo.

Mhe. Mangosongo ameongeza kuwa upimaji wa VVU ni jambo la hiyari lakini lenye umuhimu mkubwa na limekua likisaidia hata wale wanaobainika kuambukizwa VVU kuanzishiwa mara moja matumizi ya dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo na kutoa wito kwa jamii kuweka UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa kuwa ajenda ya kudumu kwenye vikao, mikutano na mikusanyiko yote kuanzia ngazi ya vijiji na kata

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameongeza kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya imejipanga kuendelea kutoa elimu ya kinga dhidi ya VVU, elimu ya lishe na jinsi ya kuishi na VVU kwa waliombukizwa sambamba na utoaji wa elimu ya UKIMWI mahala pa kazi.

Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Bw. Andrew Kapinga, kwa niaba ya Mratibu wa Huduma za UKIMWI Kinga (DACC) Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga amesema hali ya maambukizi Wilayani Mbinga kwa sasa ni asilimia 4 (4%) na kwamba jitihada mbalimbali zimekua zikichukuliwa katika mapambano dhidi ya VVU ikiwemo uhamasishaji wa tohara kwa wanaume, upimaji wa mara kwa mara na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Bw. Kapinga amefafanua kuwa sababu zinazochangia ongezeko la maambukizi ya VVU kwa Wilaya ya Mbinga kuwa ni pamoja na kushamiri kwa ngono zembe, kurithi wajane na wagane, ulevi uliopindukia, umasikini miongoni mwa jamii na imani za kishirikina.

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani hufanyika Desemba Mosi ya kila mwaka, mwaka huu yakibebwa na kauli mbiu isemayo “Zingatia Usawa, Tokomeza UKIMWI, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko” ambapo kwa Wilaya ya Mbinga maadhimisho hayo yamefanyika Kata ya Mpepai, Halmashauri ya Mji wa Mbinga.

Imeandikwa na

Salum Said, Mbinga

1 Desemba 2021


Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 May 05, 2022
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI ENEO LA KIAMILI October 13, 2021
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • VIJANA FASTAFASTA WANUFAIKA MKOPO WA BAJAJI

    April 25, 2022
  • MIRADI 9 YATEMBELEWA NA MWENGE WA UHURU 2022

    April 10, 2022
  • KAMATI YA SIASA YARIDHISHWA NA UBORA WA MIRADI MBINGA DC

    March 18, 2022
  • MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

    March 08, 2022
  • Tazama zote/kote

Video

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Christine Mndeme aagiza Halmashauri ya Wilaya kuhamiamia Kiamili kabla ya tarehe 30/10/2019
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Iringa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit