Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura Rwiza akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo leo Jumatano tarehe 12 Machi 2024 wakati alipotembelea Ofisi za Halmashauri zilizopo Kiamili kwa ajili ya kuripoti kwenye kituo chake kipya cha kazi.
Mkurugenzi Joseph Kashushura Rwiza amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma ambako pia alikua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Kufuatia mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Joseph Rwiza anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mbinga DC Juma Haji Juma ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit