Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ni miongoni mwa Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma.\halmashauri ya \wilaya ya Mbinga inapaikana Wilaya ya Mbinga, Makao yake Makuu yakipatikana eneo la Kiamili, Kigonsera takribani umbali wa kilometa 32 kutoka Mbinga Mjini na Kilometa 67 kutoka Songea Mjini na Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inapakana na Wilaya ya Nyasa kwa upande Kusini na Magharibi, Halmashauri ya Wilaya Mbinga Mjini na Wilaya ya Songea kwa upande wa Mashariki na Wilaya ya Ludewa (Mkoa wa Njombe) kwa upande wa Kaskazini
UKUBWA
Halmashauri Mbinga Vijijini ina eneo la kilometa za mraba 6,319.31, Tarafa 5, Kata 29, Vijiji 118 na Vitongoji 787 na ina Jimbo moja la Uchaguzi.
Idadi ya Watu.
Wilaya ina wakazi 353,683 kati yao wanaume ni 172,402 sawa na asilimia 48.7 na wanawake ni 181,281 sawa na asilimia 51.3 ya wakazi wote katika Wilaya,kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya 2012.Ongezeko la watu ni 2.9% . Kabila kuu ni Wamatengo ambao hujishugulisha na kilimo ,pia kuna Wangoni na Wamanda.
Hali ya Hewa
Hali ya hewa ya Mbinga ni joto la wastani wa 25°C. Wakati wa kiangazi hali ya joto inakuwa nyuzi 23oC hadi 27oC na wakati wa baridi kiasi cha joto huwa kuanzia 160C hadi 200C. Mvua hunyesha kwa muda wa miezi sita kuanzia Novemba hadi April. Wastani wa mvua ni mm. 1,200 – mm 1,800 kwa mwaka, hata hivyo katika Milima ya Umatengo wastani wa mvua hufikia mm 2,000 kwa mwaka. Aidha, kipindi cha kiangazi ni kuanzia Mei hadi Oktoba.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit